Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wahitaji dola milioni 2.3 kusaidia katika mafuriko Namibia

UM wahitaji dola milioni 2.3 kusaidia katika mafuriko Namibia

Timu ya Umoja wa Mataifa nchini Namibia inatafuta fedha za haraka dola milioni 2.3 ili kusaidia juhudi za serikali ya Namibia kutoa msaada kwa watu 60,000 walioachwa bila makazi kufuatia mafuriko makubwa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Takriban watu 200,000 wanakadiriwa kuathirika na mafuriko hayo yaliyokwishakatili maisha ya watu 65 hadi sasa kwenye mikoa ya Omusati, Oshana, Ohangwena, Okavango, Caprivi na Oshikoto. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa maeneo mengi ya vijijini hayafikiki, yamezingirwa na maji na yanaweza kufikiwa tuu kwa njia ya helkopta.

Kutokana na mafuriko yaliyojirudia kwa miaka mitatu sasa imeelezwa kuwa kina cha maji kitasalia kuwa juu kwa miezi sita ijayo huku idara ya hali ya hewa ikitabiri mvua zaidi. Pamoja na juhudi za serikali chama cha msalaba mwekundu kimekuwa msitari wa mbele katika juhudi za msaada.