Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wadau wa biashara wajadili uchumi unaojali mazingira:UNEP

Wadau wa biashara wajadili uchumi unaojali mazingira:UNEP

Wawakilishi 200 kutoka sekta ya biashara na viwanda, serikali na jumuiya za kijamii wanakutana mjini Paris Ufaransa katika mjadala wa kimataifa kuhusu kuhamia kwenye uchumi unaojali mazingira.

Mkutano huo umeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP kwa ushirikiano na kitengo cha kimataifa cha biashara na shirika la posta la Ufaransa.

Mkutano huo wa siku mbili una lengo la kutanabaisha jukumu la sekta binafsi kutoka katika mfumo wa uchumi wa sasa na kuelekea kwenye uchumi unaojali mazingira na kupunguza kiwango cha gesi ya cabon. Jason Nyakundi anaarifu.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)