Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni 2.6 wanazaliwa wamekufa kila mwaka:WHO

Watoto milioni 2.6 wanazaliwa wamekufa kila mwaka:WHO

Shirika la afya duniani WHO limezitaka serikali kutambua kwamba watoto kuzaliwa wafu ni tatizo la afya ya jamii.

Zaidi ya watoto milioni 2.6 wanaendelea kuzaliwa wakiwa wamekufa kila mwaka duniani kote kwa mujibu wa utafiti mpya uliochapishwa leo na jarida la kitabibu la Uingereza the Lancet.

WHO inasema kutoa huduma bora kwa mama na mtoto na pia kutibu maradhi kama kaswende, shinikizo la damu na kisukari kwa kina mama kunaweza kuokoa maisha ya watoto zaidi ya milioni moja kila mwaka. Dr Fredrik Froen ni kutoka taasisi ya afya ya jamii ya Norway.

(SAUTI YA DR FREDRIK FROEN)

Karibu theluthi mbili ya watoto wanaozaliwa wafu ni kutoka katika nchi kumi zikiwemo India, Pakistan, Nigeria, China, Bangladesh, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ethiopia, Indonesia, Afghanistan na Tanzania.

Jarida hilo linasema watoto wengi wanaozaliwa wafu hawawekewi kumbukumbu lakini wanahusishwa na ukosefu wa utaalamu wa huduma za afya kwa kina mama na watoto wakati wa kujifungua.