Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITU yazindua shindano la matumizi ya simu za mikononi

ITU yazindua shindano la matumizi ya simu za mikononi

Shirika la umoja wa mataifa linalohusika na mawasiliano ITU limezindua shindano maalumu ambalo litashuhudia mshindi akiondoka na kitita cha dola za marekani 10,000 iwapo atafanikiwa kubuni matumizi ya simun ya mkononi ambayo ni rafiki kwa mazingira.

Maafisa wa ITU wameeleza kuwa shindano hilo linashabaya ya kuibuliwa kwa mbinu zitakazosaidia kukabiliana na matatizo ya tabia nchi.

Mshindi kwenye shindano hilo pamoja na kuondoka na kiasi hicho cha fedha, lakini pia atapewa fursa ya kuonyesha kazi zake kwenye mkutano ya kimataifa ya mabadiliko ya tabia nchi utakayofanyika Durban Afrika Kusin mwezi disemba mwaka huu.

Ikielezea zaidi ITU imesema kuwa inamatumaini makubwa kwamba washindani watakoleza ubunifu wao na kuibuka na kitu ambacho kitatoa hamasa kwa wengi.