Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waendelea kutoa huduma katika sehemu hatari duniani

UM waendelea kutoa huduma katika sehemu hatari duniani

Utafiti uliondeshwa na Umoja wa Mataifa unaonyesha kuwa mashambulizi dhidi ya wafanyikazi wa kutoa huduma za kibinadamu yameongezeka mara tatu zaidi kwa muda wa miaka kumi iliyopita ambapo wafanyikazi 100 huuawa kila mwaka hususan kwenye maeneo yanayokabiliwa na mizozo kama vile Afghanistan, Pakistan na Somalia.

Mkuu wa huduma za kibinadamu za Umoja wa Mataifa aliye pia mkuu kwenye afisi ya shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA Valerie Amos anasema kuwa leo hii wafanyikazi wa kutoa huduma za kibinadamu wako kwenye sehemu hatari zaidi duniani.

Amesema kuwa hata kama wanakabiliwa na mashambulizi huwa wanapata njia za kutoa huduma zinazochangia katika kuokoa maisha ya watu.