Fedha zaidi zinaelekwezwa kwenye matumizi ya kijeshi:UM

Fedha zaidi zinaelekwezwa kwenye matumizi ya kijeshi:UM

Afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa nchi nyingi huwa zinatumia kiasi kikubwa cha fedha katika masuala ya kijeshi kama vile ununuzi wa silaha kuliko zinazotumia katika kupambana na umaskini, kutoa elimu kwa watoto na katika kutoa huduma bora za kiafya.

Sergio Duarte mjumbe wa Umoja wa Mataiga katika masuala ya kupunguza silaha maetoa wito kwa serikali kutenga fedha zaidi katika kutimiza malengo ya milenia. Bwana Duarte amesema kuwa bajeti za kijeshi zimeongezeka kwa nusu kwa miaka mitano iliyopita huku matumizi yote ya kijeshi yakikadiriwa kuwa zaidi ya dola trilioni 1.2 kote duniani.

Amezitaka serikali kuona uwezekano uliopo katika kudumisha usalama bila ya kutumia jeshi akiongeza kuiwa huduma bora za kiafya na elimu bora kwa wote vinaleta matumaini katika siku za baadaye.