Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kuhusu Somalia wamalizika: Mahiga

Mkutano wa kuhusu Somalia wamalizika: Mahiga

Mkutano muhimu wa majadiliano ya hatma ya Somalia ulioanza jana mjini Nairobi Kenya unamalizika leo.

Mkutano huo ulioandaliwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Somalia Balozi Augustine Mahiga umewaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo serikali ya mpito, wapinzani, wahisani na wawakilishi wa makundi ya kijamii.

Kwa mujibu wa balozi Mahiga mkutano huo ni muhimu sana kwa Wasomali hasa katika kumaliza tofauti za kisiasa , kudumisha amani na kuhakikisha usalama. Lengo lake ni kuimarisha mazungumzo baina ya serikali ya mpito ya Somalia na washirika wake. Jason Nyakundi anaripoti toka Nairobi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)