Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna haja ya kuzuia chakula kutoka Japan:WHO

Hakuna haja ya kuzuia chakula kutoka Japan:WHO

Serikali nyingi duniani zimeanza utekelezaji wa hatua za kupunguza uingizaji chakula kutoka nchini Japan zikihofia huenda kimechanganyika na mionzi ya nyuklia.

Serikali ya India imetangaza kusitisha uingizaji chakula kutoka Japan kwa miezi mitatu, huku Muungano wa Ulaya ukisema imeimarisha zaidi udhibiti wa chakula kutoka Japan. Shirika la afya duniani WHO linasema ingawa hofu ya jamii kuhusu usalama ilikuwa ya msingi lakini kwa sasa hakuna haja ya kupiga marufuku chakula kutoka Japan.

WHO inasema imeridhika kwamba hatua za usalama zimechukuliwa na serikali ya Japan ikiwa ni pamoja na kupima bidhaa zote zinazosafirishwa nje kama zimeathirika na mionzi , hatua ambazo zinatosha kulinda jamii kutokana na mionzi hiyo. Dr Maria Neira ni mkurugenzi wa afya ya jamii wa WHO.

(SAUTI YA DR MARIA NEIRA)

Ajali ya nyuklia kwenye mtambo wa Fukushima Daiichi nchini Japan imepandishwa na kufikia kiwango cha 7, lakini serikali ya Japan inasema kupandishwa huko kunatokana na kupitia upya masuala ya kiufundi na sio kwamba hali imekuwa mbaya zaidi.