Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanza kuwaondoa wakimbizi waliokwama Misrata

IOM yaanza kuwaondoa wakimbizi waliokwama Misrata

Meli iliyo na uwezo wa kubeba abiria 1000 iliyokodishwa na shirika na kimataifa la uhamiaji IOM imeondoka katika eneo la Brindisi kusini mwa Italia ili kuwahamisha maelfu watu waliokwama kwenye mji wa Misrata nchini Libya.

Meli hiyo inatarajiwa kupitia mji wa Benghazi ambapo itasheheni misaada uliyotolewa na mashirika ya kutoa misaada pamoja na wenyeji ikiwemo mablanketi, chakula, maji na madawa kabla ya kuelekea kwenye mji wa Misrata ulio kilomita 130 magharibi mwa mji mkuu Tripoli.

Maelfu ya wahamiaji wanakisiwa kukwama kwenye mapigano kati ya serikali na waasi. Jumbe Omari Jumbe afisa wa habari na uhusiano wa IOM anaeleza:

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)