Skip to main content

Pillay ashangazwa na mauaji yanayoendelea Syria

Pillay ashangazwa na mauaji yanayoendelea Syria

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameeelezea kushangazwa kwake kufuatia kuendelea kuripotiwa visa vya mauaji ya waandamanaji na vikosi vya usalama nchini Syria.

Na pia matukio yaliyoshamiri ya kukamatwa kwa watetezi wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuhangaishwa kwa waandishi wa habari. Amesema kuwa ni lazima serikali ya Syria iwaachilie huru waandishi wa habari wanaozuiliwa na iheshimu haki ya kusema.

Pillay pia ameitumia fursa hiyo kuukumbusha utawala wa Syria kuwa matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji hakujaleta utulivu katika eneo hilo.