Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa UN-HABITAT waanza Nairobi Kenya

Mkutano wa UN-HABITAT waanza Nairobi Kenya

Wajumbe kutoka sehemu mbali mbali duniani wanakutana mjini Nairobi nchini Kenya kwenye mkutano wa baraza la shirika la makaazi la Umoja wa Mataifa la UN-HABITAT ambapo masuala kadha yakiwemo bajeti na miradi ya shirika la UN-HABITAT kwa muda wa miaka miwili ijayo itajadiliwa.

Mkutano huo pia utazungumzia njia za kufadhili miradi ya ujenzi wa nyumba nafuu mijini ikizingatiwa kuwa zaidi ya nusu ya watu wote duniani wanaishi mijini na huenda idadi hii ikaongezeka zaidi kwa miaka inayokuja.

Patrick Lutabansibwa katibu katika wizara ya ardhi , nyumba na maendeleo ya makaazi nchini Tanzania ni kati ya wajumbe wanaohuhuria mkutano huo.

(SAUTI YA PATRICK LUTABANSIBWA)

Mkutano huo wa juma moja unahudhuriwa na mawaziri, maafisa wa ngazi za juu na waakilishi wengine wa serikali mbali mbali wakiwemo washirika wa shirika la UN-HABITAT ambapo pia suala la athari za mabadiliko ya hali ya hewa mijini litajadiliwa.