Balozi Mahiga aongoza mkutano wa hatma ya Somalia
Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga anaongoza mkutano mjini Nairobi Kenya wa pande tofauti nchini Somalia zilizo na nia ya kuimarisha mashauriano kati ya serikali ya mpito ya Somalia na washirika wake.
Lengo kuu la mkutano huo ni kuzisaidia taasisi za serikali ya mpito kumaliza tofauti zao kwa njia ya majadiliano ili kuuwesesha mpango wa amani kusonga mbele kwa manufaa ya watu wa Somalia.
Hata hivyo mkutano huo unaendelea kukabiliwa na shutuma huku ripoti zikiibuka kuwa serikali ya mpito nchini Somalia haijahudhuria mkutano huo.