Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walibya zaidi wakimbia ghasia na kuingia Tunisia:UNHCR

Walibya zaidi wakimbia ghasia na kuingia Tunisia:UNHCR

Zaidi ya walibya 500 wanaokimbia mzozo kwenye maeneo ya milima ya magharibi nchini Libya wanaripotiwa kuvuka mpaka na kuchukua hifadhi katika eneo la Dehiba kusini mwa Tunisia.

Kwa sasa serikali ya Tunisia inafanya jitihada za kuwapa wakimbizi hao mahitaji muhimu kama maji na umeme ambapo pia shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR kwa ushirikiano na shirika la mwezi mwekundu nchini Tunisia wanawapa msaada wakimbizi hao. Andrej Mahecic ni kutoka UNHCR:

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)

Nao wenyeji nchini Tunisia wanatoa usaidizi kwa kuwaruhusu wakimbizi hao kuchukua hifadhi majumbani mwao.