Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wateuliwa kuchunguza ukiukwaji haki Ivory Coast

Wataalamu wateuliwa kuchunguza ukiukwaji haki Ivory Coast

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limewateua wataalamu watatu ambao watachunguza madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Ivory Coast kufuatia ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa urais uliokumbwa na utata.

Kundi hilo la wataalamu litaongozwa na Prof Vitit Muntabhorn kutoka nchini Thailand ambaye hapo awali alikuwa mjumbe maalumu wa haki za binadamu nchini Korea Kusini. Cedric Sapey ni kutoka kwa shirika la haki za binadamu.

(SAUTI YA CEDRIC SAPEY)

Wanachama wengine ni pamoja na Suliman Baldo mtaalamu wa mizozo kutoka Sudan na Bi Reine Alapini Gansou ambaye ni wakili kutoka nchini Benin.