Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 500 wauawa Magharibi mwa Ivory Coast:UM

Watu 500 wauawa Magharibi mwa Ivory Coast:UM

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 500 wameuawa magharibi mwa Ivory Coast tangu mwishoni mwa mwezi Machi baada ya mauaji kutekelezwa katika miji ya Duékoué, Guiglo, Blolequin na Bangolo.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka wakati uchunguzi unapoendelea. Mkuu huyo anasema kuwa anatoa wito kwa pande husika kusitisha ghasia akisema kuwa sheria ndiyo nguzo muhimu katika kuleta mapatano. Ravina Shamdasani ni kutoka afisi ya kutetea haki za binadamu.

(SAUTI YA RAVINA SHAMDASANI)

Afisa huyo pia anasema kuwa kuwa hali na waliko wanajeshi waaminifu wa Laurent Gbagbo waliokamatwa hapo jana haijulikani.