Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuwapelekea chakula wakimbizi kwa ndege Ivory Coast

WFP kuwapelekea chakula wakimbizi kwa ndege Ivory Coast

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP linapanga kuanza operesheni ya utumiaji ndege kuwasambazia chakula mamia kwa maefu ya wakimbizi wa Ivory Coast na wale waliokimbilia nchi za jirani ambao wanakabiliwa na hali mbaya ya ukosefu chakula.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, Josette Sheeran amesema kuwa ndege yenye misaada ya kiutu itaanza kuruka katika maeneo kadhaa ikiwemo Niger, Ivory Coast na Liberia kwa shabaya ya kutawanya vyakula na mahitaji mengine kwa waathirika hao wa machafuko ya kisiasa.

Kukosekana kwa hali ya usalama na ugumu wa usambazaji huduma za kisamaria mwema kwenye maeneo kadhaa kumekwaza juhudi zilizoanzishwa na WFP ambazo zilianzishwa hapo kabla. WFP imesema pia inakusudia kusambaza bidhaa nyingine kama vyakula vyepesi ikiwemo biskuti ili kuhakikisha kwamba hakuna wakazi wanaopoteza maisha kwa njaa.