Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni miaka 50 tangu binadamu kwenda anga za mbali

Ni miaka 50 tangu binadamu kwenda anga za mbali

Leo April 12 ni miaka 50 tangu binadamu kwa kwanza kwenda kwenye anga za mbali. Mwanaanga Mrusi YuriGagarin alizunguka dunia kwa chombo maalumu cha kusafiria angani kilichoitwa Vostok .

Safari yake ilikuwa ni ushindi mkubwa kwa muungano wa Sovieti ya zamani ambao ulikuwa ukishindana na Marekani kwa kuwa nchi ya kwanza kupeleka binadamu anga za mbali.

Mazlan Othman mkurugenzi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya anga za mbali anasema safari hiyo ya anga za mbali ilikuwa ni chachu ya upelelezi zaidi wa anga za mbali.

(SAUTI YA MAZLAN OTHMAN)

Warusi na Wamarekani wamekuwa wakipeleka wanyama anga za mbali, nyani na mbwa. Na ilikuwa muhimu sana hatimaye kuweza kupeleka binadamu. Hivyo ulikuwa ni ushindani kati ya Marekamu na muungano wa Soviet na Muungano wa Soviet ulitaka kuwa wa kwanza kupeleka binadamu anga za mbali.