Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yanayoendelea Syria yanatia hofu:Ban

Machafuko yanayoendelea Syria yanatia hofu:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea hofu yake juu ya machafuko ya karibuni nchini Syria ambako taarifa zinasema waandamanaji na wanajeshi wa usalama wameuawa katika maandamano yaliyofanyika mjini Deraa Kusini mwa nchi hiyo.

Ban amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Syria Bashar al-Assad na kumwambia jinsi anavyohisi kufuatia hali ya machafuko nchini humo. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Maandamano ya safari hii ni jaribio kubwa kwa utawala wa rais Assad na linatafsiri ushawishi wa umma unaondelea sasa kwenye nchi za Afrika kaskazini ambako pia kumeshuhudiwa baadhi ya tawala zikidongoka.

Ban amewambia kiongozi huyo wa Syria kuwa tukio la  mauwaji kwa baadhi ya waandamanaji ni kitendo kisichokubalika na lazima kifanyiwe uchunguzi wa kina. Tayari rais Assad amekubali kuanzisha uchunguzi huo na kwa mujibu wa duru za vyombo  vya habari, Ban amemtia moyo kuendelea haraka na hatua hiyo.

Baadhi ya taarifa za vyombo vya habari zimearifu kuwa waandamanajai wengi wajitumbukiza kwenye vitendo vya ghasia na kuwauwa maafisa wa jeshi, jambo ambalo Ban amesisitza kuwa vitendo vya vurugu lazima viepukwe kwa jinsi yoyote.