Mkutano wa Somalia utafanyika kama ulivyopangwa:Mahiga

Mkutano wa Somalia utafanyika kama ulivyopangwa:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia balozi Augustine Mahiga leo amesema anauhakika kwamba mkutano wa ngazi ya juu wa mjadala kuhusu Somalia unaoanza kesho Aprili 12 na 13 mjini Nairobi Kenya utakuwa na matokeo mazuri.

Mahiga amesema anatumai utafungua njia ya mustakhbali wa nchi hiyo na utafuatiwa na mkutano mwingine mjini Moghadishu kama uliopendekezwa na serikali ya mpito ya Somalia.  Mahiga anasema hivi sasa washiriki wengi wameshawasili mjini Nairobi na kutokana na mikutano ya awali aliyofanya ana imani mkutano huo utakuwa na faida kubwa kwa Wasomali hasa kwenye mchakato wa amani.

Amesema lengo la mkutano huo ni kufufua mazungumzo ili mchakato wa amani usonge mbele kwani hakuna mchakato wa amani utakaofanikiwa bila kuwa na mazungumzo.