Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dhulma za mtandao dhidi ya watoto zidhibitiwe:UNODC

Dhulma za mtandao dhidi ya watoto zidhibitiwe:UNODC

Afisa wa Umoja wa Mataifa leo ameonya kwamba dhuluma kwa njia ya mtandao dhidi ya watoto zinaongezeka hasa kwa kuwa watu wengi zaidi sasa wanapata fursa ya kutumia internet.

Yuri Fedotov ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu UNODC ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za kimataifa kukabiliana na dhuluma hizo ambazo ni moja ya mfumo wa uhalifu kwa njia ya mtandao.

Amesema uhalifu mkubwa hufanyika na mara nyingine mbele ya wazazi bila kujua. Bwana Fedotov ametoa wito huo mjini Vienna kwenye mkutano ulioanza leo wa tume ya kuzuia uhalifu na makosa ya jinai. Mada kubwa zitakazojadiliwa ni pamoja na kuwalinda watoto dhidi ya uhalifu wa mtandao na juhudi za kimataifa kukabiliana na uhalifu wa kupangwa.