Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei za chakula bado hazijatengamaa duniani:FAO

Bei za chakula bado hazijatengamaa duniani:FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limesema bei za chakula duniani zimepungua kwa mara ya kwanza baada ya kupanda mfululizo kwa miezi minane.

FAO inasema msimamo wa bei unaonyesha kwamba tangu Februari mwaka huu bei zimepungua kwa asilimia 2.9 lakini limesema bado ziko juu kwa asilimia 37 ikilinganishwa na mwezi Machi mwaka 2010.

Mkurugenzi mkuu wa FAO Jacques Diouf amesema mwezi Machi mwaka huu soko limeyumba tena kutokana na matatizo ya kiuchumi hasa yaliyochangiwa na machafuko Afrika ya Kaskazini , Mashariki ya Kati na tetemeko la ardhi na tsunami nchini Japan.

Hata hivyo ameongeza kuwa kuna matumaini kwamba mambo yatakuwa mazuri kwa mwaka huu na mwaka 2012 ingawa kwa jumla bei za chakula bado zinayumba.

(SAUTI YA JACQUES DIOUF)