Skip to main content

UM wafanya operesheni dhidi ya wanajeshi wa Gbagbo

UM wafanya operesheni dhidi ya wanajeshi wa Gbagbo

Majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI jana usiku yameanza operesheni za kijeshi dhidi ya majeshi yanayomuunga mkono Laurent Gbagbo.

Operesheni hiyo imeaanza baada ya majeshi ya Gbagbo kuendelea kushambulia Umoja wa Mataifa, serikali iliyochaguliwa na raia mjini Abdijan.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameagiza UNOCI kufanya operesheni hizo ambazo zinaungwa mkono na majeshi ya Ufaransa na kuwataka watumie njia zote kuzuia majeshi ya Gbagbo kutumia silaha nzito katika mji wa Abidjan ambao ndio mkubwa kabisa nchini Ivory Coast. Majeshi ya Gbagbo yamekuwa yakifanya mashambulizi tangu Jumatano iliyopita.