Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wairaq wanataka ahadi walizopewa na viongozi wao zitimizwe asema mwakilishi wa UM

Wairaq wanataka ahadi walizopewa na viongozi wao zitimizwe asema mwakilishi wa UM

Watu wa Iraq wanataka yale waliyoahidiwa na viongozi wao yatekelezwe na mkuu wa mpango wa msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Ad Melkert anasema wanastahili kutimiziwa ahadi hizo.

Bwana Melkert ameliambia baraza la usalama hii leo kwamba mambo yanayoendelea katika ukanda huo wa Mashariki ya kati na wito wa kutaka mabadiliko ni muhimu sana.

Amesema Iraq imepiga hatua katika mabadiliko ya kuelekea demokrasia ikiwa ni pamoja na kuidhinisha katiba, kufanya uchaguzi wa kitaifa, serikali mchanganyiko na mazingira huru ya vyombo vya habari na jamii, lakini Melkert amesema hayo hayatoshi.

(SAUTI YA AD MELKERT)

"Watu wa Iraq sasa wanadai ahadi walizopewa na viongozi wao, na katika kitovu cha maandamano ambayo yamekuwa yakiendelea Iraq tangu tarehe 25 Februari 2011, ni madai muhimu wakitaka fursa nzuri za ajira, huduma muhimu na uwajibikaji. Mpaka madai hayo yatakapotimizwa, basi hatua zilizopigwa kisiasa na kidemokrasia hadi sasa zitaonekana ni bure kwa Wairaq wa kawaida.