Bachelet na Clinton wajadili mchango wa wanawake katika demokrasia

Bachelet na Clinton wajadili mchango wa wanawake katika demokrasia

Mkuu wa kitengo kipya cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulika na masuala ya wanawake Michelle Bachelet ambaye anatembelea kwa mara ya kwanza Washington amewatolea mwito maafisa wa ngazi za juu katika serikali ya Marekani kuendelea kupigania maslahi ya wanawake duniani kote.

Amesema mamlaka hizo lazima ziendelea kuwa mstari wa mbele kupigania haki za wanawake na amegusia namna ilivyomuhimu kusaidia maeneo ya mashariki ya kati na eneo la kaskazini mwa Afrika ambako yako kwenye kipindi cha mpito.

Awali mkuu huyo alikutana na waziri wa mashauri ya kigeni Hillary Clinton kujadilia masuala mbalimbali ikiwemo hali ya mambo katika nchi za Misri na Tunisia ambako wanawake wametoa mchango mkubwa kufikia mageuzi ya kisiasa.

Pia wamejadilia ustawi wa wanawake kwa nchi ya Afghanistan ambako Umoja wa Mataifa na marekani zinashirikiana kuunga mkono harakati za wanawake.