Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ivory Coast yaendelea kuzalisha wakimbizi:UNHCR

Ivory Coast yaendelea kuzalisha wakimbizi:UNHCR

Mamia ya watu wameendelea kukimbia nchini Ivory Cost na kwenda kuomba hifadhi katika nchi za jirani,wakati ambapo machafuko ya kisiasa yakiendelea kuchacha.

Kunaarifiwa kwamba zaidi ya watu 150,000 wametawanyika katika mataifa ya afrika magharibi, huku Liberia ndiyo inayopokea wakimbizi wengi zaidi wanaofikia 135,000.

Kulingana na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR baadhi yao wamepokewa wakiwa na majeraha ya kushambuliwa na risasi na hivyo kulazimika kufikishwa kwenye vituo vya afya.

Hali inavyoonekana sasa idadi ya wakimbizi inatazamiwa kuongezeka zaidi kutokana na mkwamo wa kisiasa unaendelea sasa Ivory Cost hasa katika mji mkuu Abidjan,