Skip to main content

Mtaalamu wa UM wa haki ya uhuru wa maoni kuzuru Algeria

Mtaalamu wa UM wa haki ya uhuru wa maoni kuzuru Algeria

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kutetea haki ya kutoa maoni na kusema Frank La Rue anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza nchini Algeria kati ya tarehe 10 na 17 mwezi huu kufuatia mwaliko wa serikali.

Frank La Rue anasema kuwa ziara hii itampa fursa ya kuelewa zaidi masuala ya haki ya kutoa maoni na kusema nchini Algeria kwa kukusanya habari kutoka kwa watu wanaohusika.

Wakati wa zaira yake mtaalamu huyo atakutana na maafisa wa serikali, waakilishi wa mahakama, bunge, vyombo vya habari, mashirika ya umma, Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika mengine ya kimataifa yaliyo nchini Algeria.

Bwana La Rue anatarajiwa kuwasiliwa mapendekezo yake kwenye baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa siku za usoni.