Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yanaendelea kukabiliana na changanmoto Libya

IOM yanaendelea kukabiliana na changanmoto Libya

Shirika la kimataifa la uhamaijia IOM linasema kuwa linakabiliwa na changamoto mpya katika kuweka vituo vipya kwa kuwapokea wahamiaji wanaokimbia mapigano nchini Libya ambao wanaendelea kutumia njia tofauti kutoroka mapigano hayo.

Takriban wahamiaji 8,000 bado wanaendelea kuvuka mpaka wa Libya kila siku huku karibu nusu wakielekea Tunisia na wengine wakielekea kwenye mpaka kati ya Misri na Libya , Niger na Algeria.

Kundi la IOM limewasili kwenye mji wa Faya Largeau ambapo wataweka kituo cha kuwapokea wahamiaji 1200 ambao watawasili kwa magari kutoka Sabha kati kati mwa Libya. Jean-Philippe Chauzy ni msemaji wa IOM

(SAUTI YA JEAN PHILIPPE CHAUZY)