Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yawafungisha virago zaidi wasomali:UNHCR

Mapigano yawafungisha virago zaidi wasomali:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limezitaka pande zinazopigana nchini Somalia kukoma kuyalenga maeneo waliko raia wakati mapigano katika miji mitano kusini na kati kati mwa Somalia yakipamba moto.

UNHCR inakadiria kuwa mapigano kati ya vikosi vya serikali ya mpito na wanamgambo wa Al-Shabaab yamewalazimu karibu watu 33,000 kuhama makwao kwa muda wa majuma sita yaliyopita.

Hadi sasa watu milioni 1.4 wamelazimika kuhama makwao nchini Somalia wakiwemo waliokimbia mashambulizi kwenye mji wa Dhoobley, mji ulio karibu na mji wa Liboi kaskazini mwa Kenya. Adrian Edward ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA ANDRIAN EDWARDS)