Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yataka ICC kuahirisha kesi dhidi ya raia wake

Kenya yataka ICC kuahirisha kesi dhidi ya raia wake

Wakenya watatu zaidi mashuhuri akiwemo naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta wanaotuhumiwa kwa kupanga ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 wamefika mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC mjini Hague hii leo.

Watatu hao walifika mbele ya mahakama hiyo kusomewa mashataka yanayowakabili yakiwemo ya mauaji , kuwahamisha watu pamoja na mateso kwa binadamu.

Wakati huohuo mwakilishi wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa balozi Macharia Kamau amemwandikia barua rais wa baraza la usalama la Umoja wa Matiafa akitaka kesi hizo zihairishwe.

(SAUTI YA MACHARIA KAMAU)

Kamau ameliomba baraza hilo kufanya mkutano kujadili ombi la Kenya la kutaka kesi hizo kuhairishwa. Amesema kuwa kuhairishwa kwa kesi hizo kutaiwezesha Kenya kutekeleza mabadiliko yakiwemo ya kubuni mahakama itakayoshughulikia kesi hizo.