Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Askari mamluki ni tishio kwa haki za binadamu:UM

Askari mamluki ni tishio kwa haki za binadamu:UM

Kundi la Umoja wa Mataifa linalohusika na kuchunguza matumizi ya mamluki na kufuatia visa vilivyoshuhudiwa nchini Ivory Coast na Libya limeonya kuwa bado mamluki wanatumika barani afrika ambapo wanalipwa kuwashambulia raia.

Akiongeaa mjini Geneva mwenyekiti wa kundi hilo José Luis Gómez del Prado amesema kuwa mamluki bado wanatumika katika kuwanyima watu haki zao. Flora Nducha anaarifu.

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Bwana Del Prado amesisitiza kwamba kinachowatia hofu ni taarifa za askari mamluki kujihusisha na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Na kwa ajili hiyo wito umerejewa kwa mataifa yote kuridhia mkataba wa kimataifa wa tarehe 4 Desemba 1989 unaopinga kutoa mafunzo, kuwatumia, kuwafadhili na kuwajiri askari mamluki.

Katika wiki nzima ya mkutano kudi hilo pia limejadili mswada wa mkataba kuhusu majeshi binafsi na makampuni ya ulinzi, pamoja na wataalamu kushiriki katika mjadal ujao hapo Mai 23 hadi 27 mjini Geneva mwaka huu kuona uwezekano wa kuanzisha mfumo maalumu.

Wajumbe wa kundi hilo katika mjadala ujao pia wataangalia mapendekezo ya mkataba wa kimataifa ambayo yaliwasilishwa kwenye baraza la haki za binadamu Septemba mwaka jana kuhusu suala la askari mamluki.