Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya maiti 100 zakutwa sehemu tatu Ivory Coast

Zaidi ya maiti 100 zakutwa sehemu tatu Ivory Coast

Makundi ya kutetea haki za binadamau yanayochunguza madai ya mauji na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu magharibi mwa Ivory Coast yamepata miili 100 zaidi kwenye miji tofauti kwa muda wa masaa 24 yaliyopita.

Mnamo tarehe saba mwezi huu miili 15 ilipatikana kwenye mji wa Duékoué kando na miili 229 ambayo tayari ilikuwa imezikwa baada ya kisa cha tarehe 28 na 29 mwezi uliopita . Waliouawa wanakisiwa kutoka jamii ya Guerre ambao wamekuwa wakimuunga mkono Gbagbo na ambao huenda waliuawa wakati wapiganaji wa Alassane Ouattara walipochukua udhibiti wa mji huo.

Kisa hicho kilijiri baada ya kingine cha hapo awali ambapo watu wa jamii ya Dioula waliuawa na wanajeshi wa Gbagbo waliokuwa wakiudhibiti mji wa Duekoue awali. Rupert Colville ni kutoka afisi ya kutetea haki za binadamu.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)