Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wa Ivory Coast wametiwa kiwewe kikubwa na machafuko:Amos

Watu wa Ivory Coast wametiwa kiwewe kikubwa na machafuko:Amos

Watu wa Ivory Coast wametiwa kiwewe na machafuko yanayoendelea nchini mwao amesema mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos.

Bi Amos ambaye amerejea kutoka nchini Ivory Coast na Liberia amesema jumuiya ya kimataifa lazima iongeze juhudi kutafuta suluhisho la kisiasa la mvutano uliopo baina ya majeshi yanayomuunga mkono Laurent Gbagbo na yale ya upande wa Alassane Ouattara.

Bwana Gbagbo ambaye amegoma kuondoka madarakani na kukabidhi kiti cha Urais kwa Ouattara anayetambulika kimataifa kama mshindi wa uchaguziwa mwaka jana amearifiwa kuzingirwa na kujificha kwenye kasri lake.

Bi Amos alizuru mji wa magharibi wa Duekeue ambao hivi karibuni umedhibitiwa na majeshi ambayo ni wafuasi wa Ouattara na kushuhudia majengo yaliyochomwa moto na kuharibiwa vibaya.

(SAUTI YA VALARIE AMOS)

Bi Amos amesema amesikia madai kwamba kuna mamia kama sio maelfu ya watu ambao bado wamejificha msituni na wanamgambo wanasaka watu kwa kutumia mbwa.