Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wakwama katika mapambano Misrata:UM

Maelfu wakwama katika mapambano Misrata:UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu OCHA bi Valerie Amos wameelezea hofu kubwa waliyo nayo kuhusu hali mbaya ya kibinadamu kwenye mji wa Misrata nchini Libya.

Ban amerejea wito wake kwa pande zote zinazohusika na mapigano yanayoelezewa kuwa makubwa na yanatumia silaha nzitonzito kuwalinda raia na kusitisha vita mara moja.

Bi Amos amesema watu laki tatu katika mji wa Misrata wamejikuta katikati ya mapambano ambayo yameshakatili mamia ya watu na kujeruhi wengine wengi kwa siku 40 sasa. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Maelfu ya watu wameendelea kukwama katika mji wa Misrata, wengi wao wakiwa wageni wa nchi za mbali, wakimbizi na raia wenyeji ambao wanataka kukimbia eneo hilo.

Taarifa zaidi zinasema kwamba licha ya eneo hilo kutawaliwa na hali ya hatari, lakini kuna kisanga kingine kinachowaandama kama kukosekana kwa chakula, uhaba wa maji, kutokuwepo kwa huduma nyingine za kijamii kama madawa, umeme.

Mkuu huyu wa shirika la usamaria mwema la Umoja wa Mataifa Bi Amos amesema kuwa imeingiwa na wawasiwasi mkubwa kutokana na hali inavyoendelea kuchacha