Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahanga wa mauaji ya kimbari ya Rwanda wakumbukwa

Wahanga wa mauaji ya kimbari ya Rwanda wakumbukwa

Katika siku ya leo ya kimataifa ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari ya Rwanda hapo mwaka 1994, kauli mbiu ni ujenzi wa Rwanda, maridhiano na elimu.

Akitoa ujumbe maalumu kwa ajili ya siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza serikali na watu wa Rwanda kwa kuonyesha mshikamano na utu katika kukabili athari za janga la kimbari ambalo lingeweza kuzuilika. Ban amewatia shime watu wa nchi hiyo kuendelea kuwa na umoja, upatanishi na majadiliano yanayohitajika kuponya majeraha ya moyo ya janga hilo.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Ameongeza kuwa dunia asilani haitovumilia tena ukatili wa aina hiyo na hakuna atakayeweza kukwepa mkono wa sheria kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa kwani kuzuia mauaji ya kimbari ni jukumu la kila mtu lakini pia ni jukumu la pamoja.

Nao manusura wa mauaji hayo miaka 17 baada ya kutokea wanasema wamesamehe lakini asilani hawatosahau.

(SAUTI YA MANUSURA RWANDA)