Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban kwenda Washington kuzungumza na maafisa wa serikali

Ban kwenda Washington kuzungumza na maafisa wa serikali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kesho Alhamis atakuwa mjini Washington ambako atakutana na maafisa wa serikali kujadilia masuala mbalimbali yanayohusu umoja huo wa mataifa.

Kwa mujibu wa msemaji wake amesema kuwa mara ya mwisho Ban alitombelea Washington February mwaka huu alikuwa na mazungumzo na rais Barack Obama kuhusiana na hali ya mambo nchini Libya na pia alitembelea makumbusho ya mauwaji ya Holocaust.

Katika ziara yake hiyo, Ban atakutana maafisa kadhaa ikiwemo wabunge wa seneti, maafisa kutoka wizara ya mambo ya nje na baadaye atakutana na waziri wa mambo ya nje Hillary Clinton.