Utamadunia wa kuvumiliana katika dini ni muhimu:Ban

6 Aprili 2011

Umoja wa Mataifa unasukuma mbele utu wa kuvumiliana miongoni mwa imani tofauti za kidini, na hatua ya hivi karibuni ya kuchomwa moto kitabu kitakatifu cha Koran nchini Marekani, ni eneo mojawapo ambalo umoja huo wa mataifa unasisitiza kuwa lazima jamii ziendelea kuwa na subra ya kuvumiliana.

Hayo ni maelezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati alipokutana na mabalozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya nchi za Kiislamu, OIC.

Ban amesema kuwa vitendo vya jinsi hiyo haviwezi kufumbiwa macho na kuachwa viendelea kwani jamii inapaswa kuishi kwenye mazingira ya kuchukuliana na kuvumilia utamaduni wa imani nyingine. Amezungumzia pia umuhimu wa jamii kuheshimu na kuthamini dini ya upande mwingine  kwani kwa kufanya hivyo kunajenga daraja la maenelewano na makaribiano zaidi.

Hatua ya uchomaji moto wa kitabu Koran kilichochea hasira katika mataifa kadhaa na nchini kulizuka maandamano makubwa na baadaye kushuhudiwa maafisa kadhaa wa umoja wa mataifa wakiuwawa.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter