Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chakula ni muhimu sana kwa Wasomali:Sheeran

Chakula ni muhimu sana kwa Wasomali:Sheeran

Mkurugenzi mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Josette Sheeran ameelezea matatizo wanayopitia Wasomali baada ya kufanya ziara kwenye nchi hiyo iliyokumbwa na mapigano na ukame kwa muda mrefu.

Sheeran hata hivyo amesema kuwa jitihada zinazofanywa zinalisaidia shirika hilo kuwafikia watu wanaohitaji zaidi chakula hususan wanawake na watoto.

Kwenye ziara hiyo Sheeran alikutana na akina mama waliohama makwao kutokana na kuwepo kwa ukame wa muda mrefu waliomueleza kuwa huu ni wakati mgumu zaidi katika maisha yao na jinsi familia zao zimepoteza mifugo wote.

Anasema kuwa utafiti wa hivi majuzi ulionyesha jinsi asilimia kubwa ya ubongo wa watoto wanaozaliwa katika maeneo hayo haukui kwa njia inayostahili akiongeza kuwa ikiwa wato hao hawatapata lishe inayostahili huenda wasirejee hali ya kawaida.