Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya mcheza filam Ramallah

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya mcheza filam Ramallah

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova leo ameelezea huzuni yake na kulaani vikali mauaji ya mcheza filamu Juliano Mer-Khamis aliyepigwa risasi April 4 mjini Jenin Ukingo wa Magaharibi.

Mcheza filamu huyo Mer-Khamis pia alikuwa mkurugenzi wa kituo cha sanaa cha Freedom Theatre kinachofadhiliwa na ofisi ya UNESCO ya Ramallah katika eneo la Wapalestina linalokaliwa.

Bi Bokova amesema amepokea kifo cha mwigizaji huyo wa Israel kwa huzuni kubwa kwani alikuwa mtu mashuhuri katika ulimwengu wa utamaduni Mashariki ya Kati, na mpatanishi wa amani baina ya Israel na Palestina kwani wazazi wake mmoja ni Muisrael na mwingine Mpalestina.

Juliano Mer-Khamis aliyekuwa na umri wa miaka 52, alipigwa risasi akiwa katika gari lake na mtu mwenye silaha asiyejulikana kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin kwenye ukingo wa Magharibi.