Skip to main content

Wafanyakazi wa UM wawakumbuka wenzao 40 waliokufa kazini

Wafanyakazi wa UM wawakumbuka wenzao 40 waliokufa kazini

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiongozwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon leo wamewakumbuka wenzao 40 waliopoteza maisha wiki iliyopita kwa kuweka shada la maua kwenye hafla maalumu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York.

Tangu Jumatano iliyopita Umoja wa Mataifa umepoteza wafanyakazi Haiti, Ivory Coast, saba waliokufa Afghanistan, 32 kwenye ajali ya ndege Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waliotekwa na kushambuliwa Darfur Sudan.

Akizungumza katika hafla hiyo Ban amesema vifo vya wafanyakazi hao ni vya kushtua na kutia simanzi, lakini amesema daiama Umoja wa Mataifa utashikamana .

(SAUTI YA BAN KI-MOON)