Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji zaidi ya 250 wazama Lampedusa:IOM

Wahamiaji zaidi ya 250 wazama Lampedusa:IOM

Wahamiaji zaidi ya 250 wanahofiwa kufa maji baada ya boti iliyokuwa imebeba watu 300 kuzama mapema leo maili 40 kutoka kisiwa cha Lampedusa Italia.

Wahamiaji 47 wameokolewa na wanamaji wa Italia na watatu wameokolewa na boti ya uvuvi ya eneo hilo. Boti hiyo inayosemekana kujaza watu kupita kiasi iliondoka pwani ya Libya ikiwa na wahamiaji na waomba hifadhi kutoka Somalia, Nigeria, Bangladesh, Ivory Coast, Chad na Sudan.

Wanawake 40 na watoto watano ni miongoni mwa waliokuwa kwenye boti hiyo na ni wanawake wawili tuu ndio walionusurika. Jumbe Omari Jumbe ni afisa habari na mawasiliano wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Ameongeza kuwa walionusurika walipelekwa Lampedusa kupata huduma ya kwanza na ushauri nasaha. Watu hao walinusurika baada ya kuogelea hadi pwani na wengi waliozama ni wale waloshindwa kuogelea au waliokuwa wakivutwa na abiria wenzao.