Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlinda amani wa UNAMID auawa Darfur Sudan

Mlinda amani wa UNAMID auawa Darfur Sudan

Mlinda amani wa vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID ameuawa jana Jumanne baada ya kutekwa na watu wenye sialaha.

Mwa mujibu wa UNAMID walinda amani watatu wa walitekwa kufuatia majibizano ya risasi kaskazini mwa Darfur jimbo lililoghubikwa na machafuko nchini Sudan.

UNAMID imesema kundi la watu wenye silaha walivamia gari la walinda amani hao waliokuwa wakirejea kutoka kwenye doria mjini Fata Borno jimbo la Darfur Kaskazini. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)