Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kasri la Gbagbo lashambulia mjini Abdjan

Kasri la Gbagbo lashambulia mjini Abdjan

Taatrifa kutoka mjini Abdjan nchini Ivory Coast zinasema masjeshi yanayompinga Rais Laurent Gbagbo aliyegoma kuondoka madarakani leo wameshambulia kasri la kiongozi huyo ambamo amejificha kuhofia usalama wake.

Bwana Gbagbo amekuwa na mazungumzo na Umoja wa Mataifa kuhusu usitishaji mapigano na uwezekano wa kuondoka kwake nchini Ivory Coast lakini taarifa zinasema mazungumzo hayo yaliyofanyika hadi usiku wa manane hayakuzaa matunda.

Duru za habari za Umoja wa Mataifa zinasema milio ya risasi imekuwa ikisikika kwenye kasri la bwana Gbagbo ambamo yeye na familia yake wanaaminika kuwa katika handaki linalolindwa na wafuasi wake.

Bwana Gbagbo amegoma kumkabidhi madaraka Alassane Ouattara ambaye anatambulika kimataifa kama mshindi wa uchaguzi wa Rais uliofanyika Novemba mwaka jana.

Balozi wa Nigeria kwenye Umoja wa Mataifa Joy Ogwu anasema umefika wakati wa Gbagbo kuondoka.

(SAUTI YA JOY OGWU)