Skip to main content

Israel yatakiwa kusitisha ujenzi kwenye makazi ya Wapalestina:UM

Israel yatakiwa kusitisha ujenzi kwenye makazi ya Wapalestina:UM

Mwakilishi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito kwa Israel kusitisha mipango ya ujenzi mpya wa makazi ya walowezi kwenye eneo linalokaliwa la Wapalestina.

Ametoa wito huo baada ya serikali ya Israel kuidhinisha ujenzi wa makazi zaidi ya Wayahudi Jerusalem Mashariki. Roberty Serry mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati (UNSCO) amerejea kusema ujenzi katika eneo lolote linalokaliwa ni ukiukaji wa sheria .

Pia amesema ni kinyume na mipango ya mchakato wa amani ya quartet inyojumuisha Umoja wa Mataifa, muungano wa Ulaya, Urusi na Marekani ambayo inataka kuwe na suluhisho la mataifa mawili, Israel na Palestina na waweze kuishi pamoja kwa amani na usalama na kwa kuheshimu mipaka. Jana Jumatatu Israel imeidhinisha ujenzi wa nyumba 942 kwenye eneo la Gilo ambalo ni la Wapalestina Jerusalem Mashariki.