Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM atilia shaka nafasi ya uhuru wa kujieleza Hungary

Mtaalamu wa UM atilia shaka nafasi ya uhuru wa kujieleza Hungary

Akiwa mwishoni mwa ziara yake nchini Hungary, Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuaka ya uhuru wa haki za maoni Frank La Rue, ameelezea maoni yake kuhusiana na sheria inayoshutumiwa vikali nchini humo inayobana uhuru wa vyombo vya habari.

Mtaalamu huyo amesema kuwa kupitishwa kwa sheria mpya ya vyombo vya habari kunazidisha hali ya wasiwasi na hatari zaidi ambayo itabinya uhuru wa maoni na kujieleza. Bunge la nchi hiyo mwezi uliopita lilipitisha marekebisho ya sheria ya vyombo vya habari, katika wakati ambapo shutuma juu ya sheria hiyo zikiwa juu.

Mtaalamu huyo ameeleza kuwa uhuru wa maoni na kujieleza ndiyo nguvu kubwa inayosimamisha misingi ya demokrasia hivyo ametaka mamlaka za dola kuhakikisha kwamba inaachia uwanja kwa vyombo vya habari kufanya kazi zake kwa uwazi na uhuru.