Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yahamisha raia wa Sudan Kusini toka Kaskazini

IOM yahamisha raia wa Sudan Kusini toka Kaskazini

Kiasi cha raia 7,000 waliokuwa wakiishi katika eneo la kaskazini mwa sudan wamerejeshwa upande wa pili sudani kusini kufutia juhudi zilizofanywa na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, kwa kushirikiana na kamishna ya Sudan inayohusika na utu wema.

Watu hao wakiwa wanaume kwa wanawake pamoja na familia zao ambao walikwama kwa zaidi ya miezi mitatu kandoni bandari ya mto Kosti, wamerejea kwenye maeneo yao Malakal na Juba. Ripoti zinasema kuwa watu hao walikuwa wakiishi kwa taabu kutokana na msongamano mkubwa uliokuwepo kwenye eneo hilo la bandari.

Kundi la kwanza la watu wapatao 2,988 liliwasili katika mji wa Malakal mapema mwezi uliopita wa Machi na baadaye kufuatiwa na makundi mengine.