Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa ndani zaidi ya 160,000 kuhamishwa kwa nguvu Haiti

Wakimbizi wa ndani zaidi ya 160,000 kuhamishwa kwa nguvu Haiti

Huenda wakimbizi wa ndani 166,000 wanaoishi kwenye kambi nchini Haiti wakaondolewa kwa nguvu kutoka kwa kambi hizo.

Hii ni kulingana na ripoti ya shirika la kimataifa la uhamiaji IOM inayosema kuwa kila mkimbizi mmoja wa ndani kati ya wakimbizi wane ametakiwa kuondoka kwenye ardhi ambayo wamekuwa wakiishi tangu Haiti ikumbwe na tetemeko kubwa la ardhi au waondolewe kwa lazima.

Tangu mwezi Juni mwaka uliopita wakimbizi wa ndani 234,000 wako kwenye hatari ya kuondolewa kwa nguvu kutoka kwa amaeneo wanayoishi jinsi anavyoeleza Jean Philippe Chauzy kutoka IOM.

(SAUTI YA Jean Philippe Chauzy)