Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tabala la ozoni liko katika hatari ya kuharibiwa:WMO

Tabala la ozoni liko katika hatari ya kuharibiwa:WMO

Kuharibiwa kwa tabaka Ozoni ambayo ni ngao inayoikinga dunia kutoka na miale hatari kumefikia viwango vya juu katika eneo la Arctic hali ambayo imesababishwa na kundelea kuongezeka kwa viini vinavyosababisha kuendelea kuharibika kwa tabaka hilo.

Kuendelea kuharibika kwa tabaka ozoni kunaendelea kushuhudiwa hata baada ya jitihada za kimataifa zilizofanikiwa katika kupunguza kemikali zinazosabbaisha kuharibika kwa tabaka hilo.

Hata hivyo huenda ikachukua muda mrefu kupunguza viwango vya kemikali hizo hadi kufikia viwango vya mwaka 1980 vilivyoafikiwa kwenye mkutano wa Montreal.