Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jolie ataka wanaokimbia Libya kupewa msaada:UNHCR

Jolie ataka wanaokimbia Libya kupewa msaada:UNHCR

Balozi mwema wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR Angelina Jolie ametoa wito wa kutaka wanaokimbia ghasia nchini Libya kupewa usaidizi wa kimataiafa.

Zaidi ya watu 400,000 wametoroka ghasia zinazoendelea nchini Libya kwa muda wa mwezi mmoja uliopita na kuingia kwenye mataifa jirani ya Tunisia , Misri , Niger , Algeria na Sudan huku Tunisia ikipokea zaidi ya nusu ya wakimbizi wote walioikimbia Libya. George Njogopa anaarifu

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Balozi huyo wa hisani amepongeza na kushukuru kile alichokishuhudia toka kwa wananchi wa Tunisia akida kuwa wananchi hao wamekumbatia utu wa mafanikio kwa taifa lao katika siku za usoni. Kulingna na Jolie, jumuiya za kimataifa zimefanya pakubwa kuisadia Tunisia ili kuwakwamua mamia ya wananchi waliokumbwa na hali ngumu.

Hata hivyo kuna kundi  jingine la wananchi bado wanahitaji kufikiwa na misaada ya hapa na pale na Jolie

amehaidi kuendelea kuunga mkono kuendelewa kutolewa kwa misaada hiyo. Mashirika ya umoja wa mataifa yameendelea kuchapa kazi nchini humo na tayari  watu zaidi 70, 000 wamefikishwa kwenye maeneo yao ya nyumbani wakiwa salama na amani.