Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Yemen:Pillay

Kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Yemen:Pillay

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa nchini Yemen kwa muda wa miezi miwili iliyopita kutokana na kuendelea kushuhudiwa maandamano ya kuipinga serikali.

Jana Jumatatu watu 15 waliuawa na wengi kujeruhiwa wakati vikosi vya usalama vilipowafyatulia waandamanaji risasi katika eneo Taiz kusini mwa mji mkuu Sanaa.

Mkuu wa tume ya kutetea haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa idadi kubwa ya vifo vya waandamanaji ni ishara kuwa vikosi vya usalama vinatumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji.

Rupert Colvile ni kutoka ofisi ya tume ya ya kutetea haki za binadamu ya Umja wa Mataifa

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Pillay pia anatoa wito kwa utawala nchini Yemen kukomesha vitendo vya kuwahangaisha, kuwakamata na kuwafukuza watetesi wa haki za binadamu pamoja na waandishi wa habari.