Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali nchini Libya bado ni tete:UNICEF/OCHA

Hali nchini Libya bado ni tete:UNICEF/OCHA

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa utahitaji dola milioni 310 kutoa huduma za kibinadamu nchini Libya.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa karibu watu milioni 1.5 wataathiriwa na mzozo unaoendelea nchini Libya. Kulingana na shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA na la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ni kuwa kuna uhaba wa madawa, makao na bidhaa zingine kwenye mji wa Benghazi huku idadi ya wanawake na watoto wanaowasili kwenye mipaka ikiendelea kuongezeka.

UNICEF pia inasema kuwa kuna takriban watu 2,700 kutoka Somalia , Eritrea , Iraq na kutoka utawala wa Palestina walio nchini Tunisia ambao hawana mpango wowote wa kurejea kwenye nchi zao.